Afrika Magharibi inakabiliwa na kisa chake cha kwanza cha ugonjwa wa Ebola tangu kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa huo hatari mnamo mwaka 2016, wakati maafisa wa afya wa Guinea wakiliita kama "janga" baada ya watu saba kuthibitishwa kuwa na ugonjwa huo.
Guinea pamoja na shirika la afya ulimwenguni WHO limesema wamejiandaa vyema kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, tofauti na ilivyokuwa zaidi ya miaka mitano iliyopita kwa sababu ya maendeleo mazuri kwenye chanjo.
WHO imesema itaharakisha msaada kwa Guinea na kuhakikisha inapokea dawa za kutosha, wakati nchi jirani za Liberia na Sierra Leone zikichukua tahadhari.Waziri wa afya wa Guinea Remy Lama alisema watu wanne wamefariki.