Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Muhambwe, Marehemu Atashasta Justus Nditiye kilichotokea Ijumaa tarehe 12 Feb, 2021 saa nne asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa Mhe. Spika Marehemu Atashasta Justus Nditiye alipata ajali ya gari tarehe 10 Feb, 2021 katika eneo la Nanenane Jijiji Dodoma na baadaye kupatiwa matibabu ya awali katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Aidha, Spika Ndugai aliahirisha kikao cha Bunge hadi siku ya Jumamosi tarehe 13 Feb, 2021 ili kuwapa fursa Waheshimiwa Wabunge waweze kuomboleza kufuatia msiba huo.

Vilevile, Mhe Spika aliwaeleza Waheshimiwa Wabunge kwamba taarifa zaidi kuhusu utaratibu wa kumuaga marehemu zitatolewa baadaye.

Mwenyezi Mungu ailzae roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina