Tanzania imeshiriki katika Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliofanyika kwa njia ya video. 

Katika mkutano huo moja ya agenda ilikuwa nchi Wanachama kutoa taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa katika kusaini na kuridhia mkataba wa kuanzishwa kwa Eneo Huru la Biashara ya Utatu ya COMESA-EAC-SADC. 

Katika mkutano huo Tanzania kupitia Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho imeeleza kuwa ipo katika hatua za kusaini na kuridhia mkataba huo.

Mkutano huo ulioitishwa kwa dharura pia ulilenga kupitia na kujadili rasimu ya mwongozo wa utatu wa usimamizi na ufuatiliaji wa uvukaji salama wa watu na bidhaa mipakani katika kipindi hiki cha Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19). 

Jumuiya za COMESA, EAC na SADC baada ya kugundua kuwa nchi mbalimbali ziliaandaa miongozo ya kudhibiti maambukizi ya UVIKO-19 bila kuathiri uchumi na biashara iliamua kuratibu maandalizi ya miongozo ya kikanda ili kuondokana na changamoto za biashara baina ya nchi wanachama. 

Nchi wanachama zimekubaliana kuwa mkutano uitishwe tena baada ya wiki mbili ili kujadili agaenda hii na kufikia maamuzi ya pamoja.

Katika mkutano huo kwa upande wa Tanzania ulihudhuriwa na Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Geofrey Pinda Watendaji na Maafisa mbalimbali wa Serikali