Wateja Wapendwa,
Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imetengeneza na  kusimika Mfumo wa Kielektroniki wa kushughulikia maombi ya Vibali vya Kazi. Mfumo  huu umeunganishwa na Mfumo wa Kielektroniki wa kushughulikia maombi ya Vibali  vya Ukaazi unaosimamiwa na Idara ya Uhamiaji. 

Mfumo huu wa pamoja  utamwezesha mwombaji kuwasilisha maombi ya Kibali cha Kazi/Kibali cha Ukaazi,  kulipa ada husika, kupokea taarifa na uamuzi kuhusu maombi yake kwa njia ya  mtandao kupitia akaunti yake ya barua pepe. Tarehe ya uzinduzi rasmi itatangazwa  baadaye. mwombaji wa Kibali cha Kaziutamwezesha Mwajiri yeyote anayetaka  kumwajiri Mfanyakazi wa Kigeni katika Kampuni au Taasisi yake ataweza kufanya  maombi ya Kibali cha Kazi, Kulipia maombi hayo na kupokea taarifa ya kupata au  kukosa Kibali cha Kazi kupitia mfumo. Pia ataweza kujulishwa maendeleo ya maombi  ya Kibali cha Kazi na Ukaazi kupitia akaunti yake.

Kupata huduma hizi, mwombaji atatakiwa kutembelea tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu: https://bit.ly/3aHJdfz au tovuti ya Idara ya  Uhamiaji: https://bit.ly/37DyCAi na kubonyeza kiunganishi kitakachomruhusu kuanza  kufanya maombi ya Kibali cha Kazi na Kibali cha Ukaazi. Ufuatao ni utaratibu wa  kufanya maombi ya Kibali cha Kazi na Kibali cha Ukaazi katika Mfumo huu:-

 
i.  Mwombaji wa Kibali atatakiwa kujisajiri katika Mfumo huu kwa kutumia  anuani ya barua pepe inayotumika au kufungua anuani mpya;  
 
ii.  Baada ya hatua hiyo, mwombaji atatakiwa kufungua akaunti katika  Mfumo kwa kujaza majina yake na maelezo ya kampuni au taasisi  inayomwombea Kibali;

iii. Mwombaji atatakiwa kutengeneza nywila (password) itakayotumika  kuingia katika Mfumo wakati wowote anapofanya maombi mapya ya  Kibali au anapofuatilia maendeleo ya maombi aliyokwisha wasilisha;

    Baada ya kutengeneza nywila, mwombaji atawasilisha maelezo yake na  kampuni/taasisi kwa kubonyeza kitufe cha kuwasililisha (submit) ili  kukamilisha ufunguaji wa akaunti; na
    Baada ya kukamilisha kufungua akaunti, mwomba ataweza kuingia  kwenye Mfumo na kujaza Fomu ya Kielekroniki ya Maombi ya Kibali cha  Kazi.

Vitu vya kufanya kabla ya kuanza kujaza fomu za maombi ya Kibali cha Kazi na  Kibali cha Ukaazi:

    Andaa nakala za nyaraka zote zilizothibitishwa ambazo zitaambatishwa  katika maombi na kupakiwa (uploaded) kwenye Mfumo. Nyaraka  hizo zinatakiwa kuwa na vigezo vifuatavyo:-
    a) Ziwe katika mfumo wa pdf, isipokuwa picha tu ndiyo zitakuwa  katika mfumo wa jpeg, jpg na png; na
    b) Nakala hizo laini zisizidi ukubwa wa Kilobytes 500.
    Orodha ya nyaraka zinazotakiwa kwa Madaraja yote ya Vibali vya Kazi  na Vibali vya Ukaazi inapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu  Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu: https://bit.ly/3jrVw3D na tovuti ya Idara  ya Uhamiaji: https://bit.ly/37DyCAi mtawaliwa;  

iii. Mwombaji atapakia kwenye Mfumo nyaraka zinazotakiwa kwa ajili ya  maombi ya Daraja la Kibali cha Kazi na Kibali cha Ukaazi analoomba;

    Baada ya kupakia nyaraka husika, mwombaji atawasilisha maombi yake  na kupata namba ya malipo (control number) kwa njia ya mtandao kwa  ajili ya kufanya malipo. Mfumo utatoa namba hiyo moja kwa moja;
    Mwomaji atatakiwa kulipa ada ya Kibali cha Kazi kupitia akaunti ya Benki  ya Dola za Kimarekani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na  Wenye Ulemavu au kwa njia ya mtandao kupitia VISA/Master Card;
    Kwa kampuni au miradi iliyosajiliwa katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania  (TIC) au Mamlaka ya Eneo Maalum la Uwekezaji na Mauzo (EPZA),  watatakiwa kuambatisha risiti za malipo ya ada ya uwezeshaji;  

vii. Baada ya kufanya malipo Mfumo utayatuma maombi yaliyolipiwa kwa  Kamishna wa kazi kwa uamuzi wake na Mfumo utayatuma maombi hayo  kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji pale ambapo Kamishna wa Kazi  atakuwa ametoa Kibali cha Kazi.;

viii. Kama Kamishna Jenerali wa Uhamiaji atakubali ombi la Mwamobaji basi  Mwombaji atapata taarifa (Notice of Grant) ya maombi ya Kibali cha  Ukaazi na kutakiwa kufanya malipo ya maombi hayo kwa kutumia namba  ya malipo itakayotolewa na Mfumo;

    Mwombaji atahitajika kufanya malipo ya Kibali cha Ukaazi kupitia M Pesa, Tigo-Pesa au Airtel Money au kwa kulipia kupitia akaunti ya Benki  ya Dola za Kimarekani ya Idara ya Uhamiaji kulingana na Daraja la Kibali

cha Ukaazi analohitaji na baada ya kufanya malipo hayo atajulishwa  kufika katika Ofisi za Idara ya Uhamiaji kwa ajili kumalizia hatua za  maombi;

    Maombi yatakamilishwa kwa Idara ya Uhamiaji kuchapisha Kibali cha  Kielekroniki (e-permit) kupitia Smart Card. Kibali hiki kitakuwa na taarifa  za Kibali cha Kazi na Kibali cha Ukaazi; na
    Mwombajia atachukua Smart Card katika Ofisi za Idara ya Uhamiaji.  

TAARIFA MUHIMU

  1.     Waombaji wanakumbushwa kufanya maombi yao ya Vibali vya Kazi na  Vibali vya Ukaazi kupitia tovuti za Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana,  Ajira na Wenye Ulemavu: https://bit.ly/3jrVw3D au tovuti ya Idara ya Uhamiaji:  https://bit.ly/37DyCAi na si vinginevyo;
  2.     Mwombaji lazima ahakikishe anaomba Daraja sahihi la Kibali cha Kazi na  Kibali cha Ukaazi kabla ya kufanya maombi hayo; na
  3. . Malipo ya ada ya Kibali cha Kazi na Kibali cha Ukaazi ni kwa ajili ya  mwombajia aliyekusudiwa na hayarudishwi na kuhamishika.