Maafisa 27 wa Ikulu ya Sudan Kusini wamethibitihswa kuambukizwa Corona Virus ambapo wamelazimika kuwekwa karantini.

Msemaji wa Ikulu, Ateny Wek Ateny, amesema pamoja na yeye mwenyewe, walioambukizwa wanatumikia Idara za ulinzi pamoja na huduma za mapishi na udereva.

Imeelezwa Rais Salva Kiir yupo salama lakini kuanzia sasa Serikali itadhibiti idadi ya watu wanaopaswa kukutana naye. Pia, atafanya kazi akiwa nyumbani ili kuepuka maambukizi.

Kwa mujibu wa takwimu za WHO, Sudan Kusini imerekodi visa 6,417 na vifo 85 vya COVID-19 huku waliopona wakiwa 4,014.