Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ameonyesha kuchukizwa na kitendo Cha kusuasua kwa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kinondoni Studio kuelekea Mwananyamala yenye urefu wa Km 4.2 Jambo linalopelekea usumbufu kwa Wananchi hususani wagonjwa wanaokwenda kupata huduma Hospital ya Rufaa ya Mwananyamala.

Kutokana na hilo RC Kunenge amemtaka Mkandarasi anaetekeleza Mradi huo kutoka Kampuni ya CRSG kuhakikisha anafanya kazi Usiku na Mchana ili ifikapo July 30 Barabara iwe imekamilika kwa 100% na amesema ndani ya Mwezi mmoja kuanzia leo atarudi kukagua maendeleo ya Ujenzi.

Aidha RC Kunenge amewaonya TARURA kutokumuongezea Muda Mkandarasi huyo ambapo pia amewaelekeza kuwa wakali na kusimamia kikamilifu Miradi huo.

Miongoni mwa Mambo yaliyomkwaza zaidi RC Kunenge ni kuona adi kufikia Sasa Muda wa Mradi umefikia 62% lakini kazi iliyofanyika ni 16% huku wahusika wakitoa sababu dhaifu.

Kwa upande wake Makamu Mhandisi Mshauri wa Mradi huo kutoka Kampuni ya HP Gauf Wile John amemuahidi Mkuu wa Mkoa kuwa maagizo aliyotoa watayatekeleza kwa Wakati.

Ujenzi wa Barabara ya Kinondoni studio kuelekea Mwananyamala yenye urefu wa Km 4.2 inatekelezwa na Mkandarasi kutoka Kampuni ya CRSG.