Staa wa muziki wa Rap kutoka Nchini marekani Bobby Shmurda ameachiliwa kutoka gerezani Februari 23, 2021.
Rapa wa Kundi la Migos Quavo tayari ameenda kumchukua Rapa huyo kwa ndege yake binafsi kama alivyoahidi.
Siku ya leo itakuwa ya furaha zaidi kwa Mama wa Bobby Shmurda Leslie Pollard ambaye amekuwa akiisubiri tarehe ya leo kwa hamu sana, Leslie siku jana aliiambia TMZ kuwa mara Bobby atakapoachiliwa kutoka gerezani kutakuwa na hafla ndogo kufurahia chakula cha jioni na familia yake.