Rais wa Marekani Joe Biden atakuwa rais wa kwanza wa Marekani kuhudhuria mkutano wa usalama wa Munich wiki ijayo, ambao utafanyika kwa njia ya mtandao kutokana na janga linaloendelea la virusi vya corona. 

Mkutano wa usalama wa Munich ni mmoja ya matukio muhimu ya kila mwaka yanakojadiliwa masuala ya kimataifa ya usalama. 

Mkutano huo wa wataalamu wa usalama ulikuwa umepangwa awali kufanyika kuanzia Februari 19 hadi 21, lakini sasa utafanyika kwa njia ya mtandao na utadumu kwa saa chache tu. 

Mkuu wa mkutano huo, Wolfgang Ischinger, ameliambia shirika la habari la Ujerumani DPA, kwamba alipokea habari za kukubali kwa Biden kutoka ikulu ya White House, na kuzitaja kuwa za faraja. 

Kwa mujibu wa Ischinger, uamuzi wa Biden kushiriki mkutano huo unaashiria kwamba Ujerumani ni muhimu kwa Biden.