Rais John MagufuliI amepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye amefariki dunia leo Jumatano, Februari 17, 2021, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.  Natoa pole kwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mwinyi, familia, Wazanzibari, wanachama wa ACT-Wazalendo na Watanzania wote. Mungu amweke mahali pema peponi, Amina” ameeleza MagufuliI.

Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi ndiye ametangaza kifo cha Maalim Seif ambapo amesema amefariki dunia majira ya saa 5:00 asubuhi hospitalini hapo. Mwinyi pia ametangaza siku saba za maombolezo.