Polisi Nchini China imesema inawasaka Watu wanaotengeneza chanjo bandia za Corona ambapo inaripotiwa kuwa Mtandao huo wa kihalifu umekua ukitengeneza chanjo feki tangu September Mwaka 2020.

Polisi kutoka maeneo ya Jiangsu, Beijing na Shandong wamewakamata zaidi ya Watu 80 waliohusika katika utengenezaji wa zaidi ya dozi feki Elfu 3 za chanjo ya Corona.

“Wanapata faida kubwa, wanachanganya majimaji yenye chumvi ndani ya sindano ili kutengeneza chanjo bandia za virusi vya corona na kuziuza kwa bei ya juu” - Polisi.