Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ana muda wa hadi leo Jumanne kuwasilisha hoja rasmi za utetezi katika mashitaka yanayomkabili, wakati baraza la seneti likitarajiwa kusikiliza kesi hiyo baadaye mwezi huu. 

Rais huyo wa zamani alishitakiwa katika baraza la wawakilishi lenye idadi kubwa ya Wademocrats kwa kuchochea uasi, kufuatia tukio la wafuasi wake kuvamiwa majengo ya bunge mnamo Januari 6. 

Ikiwa atapatikana na hatia katika seneti, maseneta wanaweza kupiga kura nyingine ya kumzuia Trump kushiriki siasa katika siku za usoni. 

Trump amedokeza uwezekano wa kuwania urais tena mwaka 2024. Mchakato rasmi wa kusikiliza kesi yake utaanza Februari 9. 

Kiongozi wa wachache katika Seneti Mitch McConnel kutoka chama cha Republican alitoa ombi la kucheleweshwa kuanza kwa kesi ili kumpa muda Trump wa kujenga hoja za utetezi.