Mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) kutoka Kijiji vha Itebulanda wilayani Urambo Justina Yona akionyesha jana shamba lake la zao la karanga ambalo amelilima kwa kutumia fedha za TASAF anazopata.

NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA
MATUMIZI sahihi ya fedha za Mpango wa kunusuru Kaya maskini zimesaidia mama mwenye familia ya watoto 15 Justina Yona  wa Kijiji cha Itebulanda wilayani Urambo Mkoani Tabora kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha na kuzalisha ziada kwa ajili ya kuuza.

Justina alitoa kauli hiyo jana wakati wa ziara ya viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) Makao makuu waliongozana na waandishi wa habari kuangalia mafanikio mbalimbali waliopta walengwa wa TASAF kutoka na fedha wanazopata.

Alisema aliweza kupata kiasi cha shilingi 40,000 mara mbili kutoka  TASAF na kutumia fedha hizo kwa ajili ya kulima ekari zaidi ya saba zikiwemo za mahindi,karanga , mpunga  na tumbaku nakufanikiwa katika mwaka uliopita kuzalisha zaidi magunia 135 ya mazao mbalimbali.

Justina alisema katika ekari 3 za mpunga alipata gunia 60,ekari 3 za Mahindi alipata gunia zaidi ya 60 na ekari moja ya  Karanga alipata gunia 15 na alilima tumbaku na pia aliweza kuzalisha mafuta na Mawese kutokana kwa kutumia fedha za TASAF na kupata kiasi cha shilingi 100,000/= kila anapokamua mafuta.

Alisema na kutumia fedha hiyo katika shughuli za kilimo pia fedha hiyo ameweza kununua mifugo mbalimbali ikiwemo wanyama kazi ambao wanamsaidia katika shughuli mbalimbali.

“Fedha inayotolewa na TASAF haijirishi uchache wake wala wingi ni akili yako ndio inayoweza kukufanya upige hatua katika maendeleo … mimi nimeweza kutumia  fedha kununulia bati na kujenga nyumba na kutengeneza mashine kwa ajili ya kukamua mafuta ya mawese…wanaopenda anasa na starehe ndio wanalalamika kuwa fedha hiyo ni kidogo lakini sio kweli” alisema

Alisema baadhi ya walengwa wamekuwa wakipata fedha hiyo na kujielekeza kwenye anasa na starehe badala ya kuanzisha miradi ya maendeleo ambayo itawasaidia wao na familia zao.

Naye Espius Kalumanzila alisema kwa kutumia fedha za TASAF aliweza kununua mbegu za miwa na kuanzisha shamba la miwa ekari 1 na kupanda miche ya Migomba 30 na ekari 2 za Mahindi ambayo fedha inayotokana na mazao hayo imekuwa ikimsaidia katika mahitaji mbalimbali.

Alosema lengo lake ni kuhakikisha kuwa anakushanya fedha za kutosha kwa ajili ya kuboresha makazi kwa kujenga nyumba ya kisasa,na ununuzi wa pikipiki kwa ajili ya huduma ya usafiri .

Katika hayia nyingimne Afisa habari Estom Sanga amewataka walengwa ambao ni wazazi na walezi wa watoto wanaonufaika na fedha za TASAF kuhakikisha watoto wao wanahudhuria shule bila kukosa na wale wanatakiwa kwenda Kliniki wanapelekwa kama inavyotakiwa ili kuepuka kupewa adhabu ya kukatwa fedha za mpango huo kwa kushindwa kutimiza masharti.

Alisema baadhi ya wazazi wamejikuta wakipata fedha pungufu kwa sababu ya kushindwa kusimamia watoto wao ili waweze kuhudhuria masomo yao na wengine wandele Kliniki.

Alisema TASAF inalengo pia la kuhakikisha linandaa rasilimali watu wenye elimu na afya bora ambao wataweza kushiriki vema katika ujenzi wa Taifa.