Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amefanya mazunguzo na mwenzake wa Saudi Arabia na kujadili juhudi za kidiploamsia za kumaliza vita nchini Yemen pamoja na kuimarisha ulinzi wa Saudi Arabia. 

Duru za habari kutoka pande zote mbili zimearifu kuwa Blinken na Mwanamfalme Faisal Al Saud wamezungumzia umuhimu wa kutafuta suluhisho la kisiasa kwa vita nchini Yemen. 

Saudi Arabia inaongoza muungano wa kijeshi unaoendesha operesheni zake nchini Yemen tangu mwaka 2015 ukiunga mkono vikosi vya serikali vinavyopambana na waasi wa Houthi wenye mafungamano na Iran. 

Hata hivyo Marekani imetangaza kusitisha ufadhili wake kwenye operesheni hizo za kijeshi na wiki iliyopita rais Joe Biden alimteua mjumbe maalum wa Marekani kwenye mzozo wa Yemen akiashiria nia ya kutumia njia za kidiplomasia kumaliza mzozo huo