Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani jana  tarehe 21 Februari, 2021 katika ziara yake kwenye mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere megawati 2115, amesema zoezi la kujaza maji ya kufua umeme katika bwawa litaanza 15 Novemba 2021.

Dkt. Kalemani amewaomba wadau mbalimbali hususani viongozi kuhakisha wanalinda vyanzo vya maji ili kuweza kupata maji ya kutosha.

Akitoa wito kwa wananchi wote wanao lima maeneo ambapo kunavyanzo vya maji, Dkt. Kalemani amewaomba walime kilimo ambacho hakitaleta athari ya upatikanaji wa maji katika bwawa la Julius Nyerere, yatakayo tumika kuzalisha Megawati 2115.

Katika ziara hiyo ameagiza ufanisi wa kusimamia Mkandarasi usiku na mchana ili kuhakikisha anamaliza mradi kwa wakati.

” Mkandarasi ni lazima aongeze wafanyakazi na vifaa vyote vilivyo bandarini hakikisheni vinafika kwenye mradi na kufungwa kwa wakati”.

Dkt. Kalemani ameagiza TANESCO kuanza ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme 400kv kutoka rufiji hadi chalinze ili mradi utakapo kamilika umeme uweze kusafirishwa na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere una tegemewa kuzalisha takribani megawati 2115.