Rais  John Magufuli ametengua uteuzi wa mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Aron Kagurumjuli.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ta Rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa kiongozi mkuu huyo wa nchi ametengua uteuzi huo  Jumanne Februari 16, 2021.

Inaeleza kuwa uteuzi wa mkurugenzi mwingine wa manispaa hiyo utafanywa baadaye.