SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF), limetangaza rasmi kuachana na kocha wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Akizungumzia uamuzi huo, Ofisa habari wa TFF Clifford Marion Ndimbo amesema wanamshukuru kocha huyo, na tayari mchakato wa kumsaka mbadala wake umeanza ambapo atatangazwa muda wowote kuanzia sasa.