Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ameihimiza Marekani kuiondolea vikwazo vyote nchi yake iwapo Marekani inaitaka Iran izingatie makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati yake na nchi zenye nguvu ulimwenguni. 

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alisema kwenye televisheni ya taifa kwamba Marekani inapaswa kuondoa vikwazo vyake dhidi ya Iran kabla ya nchi hiyo kuanza tena kufuata makubaliano yaliyofikiwa kati yake na nchi zenye nguvu ulimwenguni. 

Khamenei mwenye umri wa miaka 81, ndiye kiongozi mwenye uamuzi wa mwisho juu ya mambo yote ya serikali nchini Iran na ndiye aliyedhinisha juhudi za kufikia makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015.