Kwa mujibu wa data za mtandao zilizotolewa na shirika linalofuatilia huduma za mitandao NetBlocks, huduma za mtandao wa Internet zimerudhishwa kwa kiasi nchini Myanmar. 

Kampuni hiyo ya Netblocks imesema upatikanaji wa huduma ya mtandao ilifikia asilimia 14 ya viwango vya kawaida na hivyo mitandao ya kijamii bado haiwezi kufikiwa. 

Licha ya taifa hilo kukosa huduma ya mtandao kwa siku kadhaa hatua hiyo haikuzuia kufanyika maandamano makubwa kupinga mapinduzi ya jeshi yaliyomwondoa uongozini Aung San Suu Kyi. 

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia maswala ya haki za binadamu nchini Myanmar, Tom Andrews amesema kuzuia huduma za mitandao ni ukiukaji wa haki za binadamu.