Dunia imekuwa kama Kijiji kwa sasa ukilinganisha na miaka ya nyuma, upatikanaji wa habari mbalimbali umekuwa ni rahisi sana basi kama ni faida au hasara tuzihamishie kwenye ukuaji wa teknolojia. Ukuwaji wa teknolojia umepelekea kampuni mbalimbali za mawasiliano na za simu kama Infinix na Tigo kuunganisha nguvu kuhakikisha kila Mtanzania anaufurahia Ulimwengu wa kidigitali kupitia Infinix HOT 10 Play. 


Infinix HOT 10 Play ni simu mpya na sifa yake kuu ikiangukia kwenye mAh 6000 za battery zenye kudumu na chaji kwa muda mrefu na kwa sasa inapatikana katika maduka yote ya simu ikiwa na ofa ya GB18 kutoka Tigo.  


Infinix Hot 10 Play sifa zake ziliwekwa wazi rasmi kupitia mtandao wa kijamii @infinixmobiletz 28/1/2021 na jana kuzinduliwa rasmi Infinix ikishirikiana na Tigo. 
     


Afisa  Mahusiano Infinix na Mkumbo Myunga kutoka Tigo wakati wa uzinduzi wa Infinix HOT 10 Play. 


“ni simu ya kila mtu, ni simu rafiki kwa wenye kipato cha kati na cha chini, pia ni rafiki kwa wanaofikiria kuingia katika ulimwengu wa simu janja kwani ni rahisi kutumia na inadumu na chaji kwa muda mrefu”alisema Aisha Karupa, Afisa Mahusino Infinix. 


Furahia ufanisi wa Helio G35 processor unapocheza games na utendaji wake katika application mbalimbali pasipo simu kupata moto. uwezo wa kuhifadhi vitu/kumbukumbu ni mkubwa. Hot 10 Play inaujazo wa 2GB/32GB na 4GB/64GB zenye nafasi kubwa kwa uhifadhiaji kumbukumbu nyingi sana kama vile picha, video, mziki na kadhalika.
                                             
HOT 10 Play ina wigo mpana wa kioo cha nchi 6.82 na kamera yenye selfie 8MP na MP13 nyuma zenye kupiga picha vizuri pasipo kuhofia aina ya mazingira au wakati.
.
Infinix HOT 10 Play inapatikana katika maduka ya Tigo na Infinix nchini kote.
Kufahamu zaidi bidhaa zao gusa HAPA  
 
 
Kwa MAWASILIANO:
074460622