Kulingana na utafiti, chanjo dhidi ya virusi vya corona iliyotengenezwa nchini Urusi Sputnik V ina ufanisi wa zaidi ya asilimia 90. 

Kulingana na utafiti huo uliochapishwa na jarida mashuhuri la Uingereza "The Lancet", chanjo hiyo imethibitishwa kuweza kumlinda binadamu kwa asilimia 91.6 dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 katika awamu ya tatu na ya mwisho ya majaribio. 

Aidha chanjo hiyo pia imetajwa kuwa ilivumiliwa vyema na watu walioshiriki utafiti. 

Tangu mwezi Desemba, Urusi ilianza kuwachanja watu walio hatarini zaidi kupata ugonjwa huo, na mnamo mwezi Januari ilianzisha kampeni kubwa zaidi ya kutoa chanjo hiyo.