Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Dkt. Bashiru Ally kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kuanzia leo Februari 26, 2021.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Bashiru alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Dkt. Bashiru anachukua nafasi ya Balozi John Kijazi aliyefariki dunia Februari 17 mwaka huu.

Wakati huo huo, Rais amemteua Dkt. Bashiru Ally kuwa Balozi.

Kiongozi huyo mteule ataapishwa Februari 27, 2021 saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.