Samirah Yusuph
Bariadi. Imeelezwa kuwa matamko na nyaraka zinazotolewa na viongozi wa madhehebu mbalimbali nchini inapaswa yatolewe na wizara ya afya kwa sababu matamko hayo yanatengeneza taharuki na hofu katika jamii.

Hayo yameelezwa februari 20, na Askofu Mark Walwa Malekana ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa adventist sabato nchini alipokuwa katika ibada maalum ya maombi Nchi nzima katika kanisa la Sima Adventist church lililopo wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.

Amesema kuwa Ulimwengu umegubikwa na magonjwa ya ajabu, hivyo sio jambo la busara kwa viongozi wa dini kutoa matamko na takwimu zisizothibitika  .

"Hofu ni zaidi ya tatizo lenyewe, hofu inaweza kuondoa maisha hivyo yapaswa wananchi waondoe hofu na kujipa moyo pamoja ujasiri na  waendelee na shughuli za kila siku bila woga...

Kwa Kuzingatia kanuni za afya na kuzifanya kuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku pamoja na kufuata miongozo na maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya itawakuwa ni tiba tosha".

Akizungumza na waumini Mzee wa kanisa zacharia Mageni
aliwataka waumini kuimalika na wasitikisike wazidi kutenda kazi ya bwana kwa siku zote na kuwa na imani katika kipindi hiki cha kupambana na magonjwa ya mlipuko.

"Kwa kuzingatia mahitaji ya mambo binafisi hivyo ni vyema kujikabidhi kwa Mungu, unapokuwa katika mikono salama ya bwana unakuwa hauna hofu".

Aidha katika siku tatu za maombi ya kuliombea taifa katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya covid -19 baadhi ya waumini katika kanisa hili wameeleza kuwa kwa licha ya maombi pia wamejikita kwenye kuhakikisha wanafuata kanuni za afya ili kijikinga na virusi hivyo.

"Ni wakati wa maombi lakini unapomuomba Mungu akusaidie  inabidi ujisaidie mwenyewe hivyo ni lazima kujikinga kwa kujiwekea mazingira safi na kuepuka kushikana mikono na hata kutumia vitakasa mikono." Alisema Juliana Lucas.