Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
TATU Bakari Hassan ,mkulima mwenye miaka 55 ,amejeruhiwa mguu wake wa kulia kwa kupigwa risasi akiwa shambani kwake ,baada ya kudhaniwa kuwa yeye ni nyani.


Jeshi la polisi mkoani Pwani ,linamshikilia mkulima Mhina Mrisho Ally (47)anaedaiwa kumjeruhi mkulima huyo.


Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa ,ameeleza,pia mtuhumiwa Mrisho alipokwenda kupekuliwa nyumbani kwake alikutwa na bunduki mbili aina ya gobore ambazo anazimiliki kinyume na sheria.


Wakati huo huo, jeshi hilo linawashikilia wahamiaji haramu sita ,raia wa Malawi, waliokuwa wakisafirishwa kutoka Mbeya kwenda Dar es salaam,kinyume na sheria huku wakiwa wameingia nchini bila vibali.


Wahamiaji hao haramu wamekamatwa eneo la Tanita, Kibaha pamoja na dereva wa gari namba T.703 DTR aina ya Toyota hiace jina limehifadhiwa mkazi wa Uyole Mbeya.


Wankyo alieleza,  wahamiaji hao walikuwa wanapelekwa Dar es salaam kufanya kazi ya kuuza bar na kusuka..


Alitoa siku saba kwa wale wote wanaomiliki silaha bila vibali kuzisalimisha silaha hizo na wakibainika katika operesheni za kipolisi basi hatua kali zitachukuliwa.


Pia alikemea madereva wanaohusika kusafirisha wahamiaji haramu kuacha Mara moja na wakikamatwa dola itachukua mkondo wake.