MABINGWA wa kihistoria Nchini timu ya Yanga imejiwekea rikodi nzuri katika
mashindano ya Mapinduzi kwa kutoruhusu kufungwa bao hata moja hadi sasa wakai
mashindano yanayoendelea katika hatua ya Nusu fainali.
Katika Michezo 2 iliyocheza Yanga walitoka sare ya 0-0 mbele ya Jamhuri
kisha kuwafunga bao 1-0 Namungo, ambapo ndio timu pekee msimu huu katika
Mashindano hayo kumaliza dakika 180 (michezo 2) pasipo kuruhusu lango lake kuguswa.
Hata hivyo Yanga kwa msimu wa 15 wa Mashindano ya Mapinduzi imeweka rikodi ya kuwa
timu ya kwanza kujihakikishia kutinga hatua ya Nusu fainali baada ya kumaliza
michezo miwili na kuwa na alama Nne na kuongoza kundi A,lenye Timu ya Namungo na
Jamuhuri ya Pemba.
Mashindano hayo yaloshirikisha timu 9 mwaka huu timu zote 8 zimeruhusu
lango lao bao isipokuwa Yanga pekee.
Hatua ya nusu Fainali ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi yamechezwa LEO katika
Dimba hilo la Amani ambapo Yanga dhidi ya Azam saa 10: 15 jioni huu Wekundu
wa Msibazi Simba dhidi ya Namungo saa mbili na robo usiku.
zitachezwa