CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga leo ameshuhudia vijana wake wakisepa na pointi tatu mazima mbele ya Namungo FC kwa ushindi wa bao 1-0, kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Amaan.


Shukrani kwa Haruna Niyonzima aliyekuwa nahodha kwenye mchezo huo baada ya kupiga faulo ya iliyokutana na guu la Zawad Mauya dakika ya 20 na kupachika bao la ushindi.


Ushindi huu ni wa kwanza kwenye Kombe la Mapinduzi kwa kuwa mchezo wa ufunguzi ililazimisha sare ya bila kufungana na Jamhuri uliochezwa Uwanja wa Amaan.


Namungo inabidi wajilaumu wenyewe kwa kushindwa kupata bao Kwenye mchezo huo kwa kuwa walipata nafasi tano za wazi  ambapo Bigirimama Blaise alikosa tatu, Abdulhalim Humud alikosa nafasi moja huku nyota mpya Eric ambaye yupo Kwenye majaribio alikosa nafasi moja ya kufunga.


Dakika 90 zilikuwa ni za nguvu mwanzo mwisho ambapo jumla kadi tatu za njano zilitolewa kwa Yanga zilikwenda kwa Mauya na Said Juma kwa Namungo ni Jaffary Mohamed.


Kipa namba mbili wa Yanga, Farouk Shikalo anakusanya clean sheet yake ya pili kwa kuwa mchezo wa kwanza hakuokota mpira nyavuni na  jana ameokoa hatari tatu.