WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Selemani Jafo amezitaka halmashauri 9 ambazo hazijatoa asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya wanawake,vijana na walemavu  kuhakikisha wanapeleka fedha hizo ndani ya wiki mbili.

Aidha,amewataka wakurugenzi wa halmashauri hizo isipokuwa ya Chalinze, siku ya Jumatatu kuwasilisha maelezo kwa Katibu Mkuu Tamisemi Mhandisi Joseph Nyamhanga wakieleza sababu ya kutotoa fedha hizo.

Akitoa taarifa ya hali ya ukusanyaji wa mapato ndani ya halmashauri na matumizi yake kwak ipindi cha nusu mwaka 2020/2021  jijini Dodoma ,Jafo amesema katika kipindi hicho halmashauri zilitoa mikopo kiasi cha Shilingi Bilioni 22.33 kwa makundi hayo ikiwa ni asilimia 35 ya bajeti wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ambayo ni Shilingi Bilioni 64.46.

Akielezea hali ya ukusanyaji wa mapato waziri Jafo amesema ameutaja mkoa wa Katavi kuwa kinara kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani yaliyokusanywa na mkoa wa Dar es salaam ukiongoza kwa kigezo cha pato ghafi ambalo ni wingi wa mapato ya ndani yaliyokusanywa.

Ametaja baadhi ya changamoto zilizojitokeza katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kipindi hicho kuwa ni baadhi ya halmashauri kutegemea zaidi chanzo cha ushuru wa mazao na hivyo kushindwa kufikia malengo kutokana na kutokulipwa kwa wakati na baadhi ya halmashauri kujiwekea makisio kwenye vyanzo ambavyo hazina uhakika wa kukusanya.

Halmashauri hizo ni halmashauri ya Wilaya ya Kakonko,Kigoma Ujiji,halamshauri ya wilaya ya Uvinza ,halmashauri ya mji wa Nanyamba, ni Tandahimba dc, Chalinze,Sumbawanga dc,Madaba dc na Mbinga dc.