Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), inawachunguza Watumishi 23 wa Taasisi ya Mifupa Muhimboli ( MOI) kitengo cha Famasia, kwa tuhuma ya uchepushaji wa dawa zenye thamani ya shilingi bilioni 1.2.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia JeneraliJohn Mbungo amesema uchunguzi wa kuwabaini Watuhumiwa hao ulianza mwaka 2018 hadi mwaka huu kwa ushirikiano na MOI na TAKUKURU.

Katika hatua nyingine Brigedia Jenerali Mbungo amefanya mabadiliko ya Watendaji ndani ya taasisi hiyo, lengo likiwa ni kuongeza ufanisi.

Pia amewaambia Waandishi wa habari kuwa, wameanzisha kitengo cha TAKUKURU kinachotembea, kitakachokuwa kikisikiliza na kutatua kero za Wananchi poppte walipo.