Wanajeshi wameondoka kwenye makazi ya kiongozi wa Upinzani nchini Uganda Bobi Wine .Siku ya Jumatatu Mahakama iliamuru jeshi na polisi kuondoka kwenye makazi yake.

Awali jeshi lilisema kuwa litatii uamuzi wa mahakama. Bobi Wine hajaondoka kwenye makazi yake yaliyo kando ya mji wa Kampala, tangu alipopiga kura kwenye uchaguzi siku 11 zilizopita.

Waandishi wa habari wa gazeti la Daily Monitor wamesema upelekaji wa jeshi na polisi ulikuwa umeimarishwa kwenye barabara inayoongoza kuelekea kwenye makazi ya Bobi Wine na vituo vya ukaguzi vimeongezeka.

Magari mawili yaliyokuwa yamewabeba waandishi wa habari kuelekea nyumbani kwa Bobi Wine walizuiwa na kuamriwa kurejea walikotoka.

 

-BBC