Waandaaji wa Tuzo za Muziki za Billboard wametangaza Tarehe rasmi ya hafla ya utoaji wa Tuzo hizo Billboard Music Awards kwa mwaka 2021 ambayo ni Mei 23, 2021

Mwaka jana Tuzo hizo zilitolewa kwa kuchelewa ( Oktoba 14) baada ya tarehe ya mwanzo kuahirishwa kutokana na janga la COVID-19, Post Malone ndiye Msanii alishinda Tuzo nyingi 2020 akitwaa jumla ya tuzo tisa ikiwa ni pamoja na Tuzo ya msanii wa bora wa mwaka na Tuzo ya msanii bora wa kiume.