Utawala wa Rais Donald Trump umeirudisha Cuba katika orodha ya ‘nchi zinazofadhili ugaidi‘ na kuiwekea vikwazo vipya vinavyoweza kukwamisha ahadi ya Biden kufufua uhusiano na serikali hiyo ya kikomunisti.

Waziri wa Mambi ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, ametangaza hatua hiyo jana Jumatatu akitaja ushirikiano kati ya Cuba na waasi wa Colombia.

Aidha sababu nyingine ni ushirikiano wa Cuba na serikali ya siasa za mrengo wa kati ya Venezuela pamoja na hatua ya Cuba kuwakaribisha wakimbizi wa Marekani kuwa miongoni mwa sababu zilizowafanya kuchukua hatua hiyo.

Suala la kuitangaza Cuba kuwa taifa linalofadhili ugaidi limejadiliwa kwa miaka mingi na ni miongoni mwa hatua kadhaa za mwisho za sera ya nchi za nje ambazo utawala wa Trump unafanya kabla ya Biden kuchukua urais Januari 20.