Waandamanaji nchini Marekani wanatarajiwa leo kukusanyika nje ya majengo ya serikali kuunga mkono madai yasiyo ya msingi ya rais Donald Trump ya kuibiwa kura kwenye uchaguzi uliopita, huku vikosi vya usalama vikijiandaa na machafuko yanayotarajiwa kutokea nchini humo.

 Zaidi ya majimbo kumi yameviweka tayari vikosi vya walinzi wa kitaifa kusaidia kuyalinda majengo ya bunge la Marekani, Capitol Hill kufuatia tahadhari kutoka kwa shirika la upelelezi la FBI la kitisho cha waandamanaji waliojihami kwa silaha.

Kuimarishwa kwa ulinzi kote nchini humo kunafuatia shambulizi baya kabisa kwenye majengo ya bunge mjini Washington Januari 6 lililofanywa na wafuasi wa Trump na wenye misimamo mikali na miongoni mwao wakitoa mwito wa kuuawa makamu wa rais Mike Pence aliyesimamia kuthibitishwa kwa rais mteule Joe Biden.