Mwaka 2020 umekuwa mwaka wa ushindani mkubwa sana kwenye tasnia ya muziki hasa bongo fleva hapa nchini nah ii imetokana na kuwa mwaka wenye kazi bora sana za muziki wa bongo fleva .


Miaka iliyopita kulikuwa na kilio cha wasanii na wadau kuhusu wasanii kutoa album tena sio album tuu bali album zenye nyimbo bora.


Lakini mwaka huo wa 2020 ndio ulianza kutambulisha album bora na zenye nyimbo bora kutoka kwa wasanii lakini lazima tukubali kabisa album ya Msanii Harmonize (AFRO-EAST) ndio moja ya ingizo bora kabisa la album na lenye nyimbo hit karibu zote na ni ukweli kabisa Harmonize alijipanga kabisa kwenye album yake kuanzia Audio na Video bila kusahau utambulisho wa album yake.




Lakini wakati watu wakiendelea ku enjoy album bora kabisa kutoka kwa Harmonize kuelekea mwishoni mwa mwaka jana 2020 kumekuwa na ujio wa album kadhaa za wasaniii kama “Asante ya Barnaba na Fashion Killer ya –Jux” Lakini kuelekea mwisho mwaka 2020 December 24 Msanii DARASA (CMG) alituletea album yake inaitwa “SLAVE BECOMES KING”


Album ya darasa haikuwa na kelele nyingi na matangazo mengi kama wasanii wengine nachelea kusema kama ilikuwa sahihi au lah kwani biashara zina mbinu nyingi na matangazo lazima.


Album ya Darasa inaweza isiwe na hit songs nyingi sana kama ya Harmonize kwa maoni yangu lakini nina hakika ni album ambayo itakuwa na nyimbo zitakazo tamba kwa muda mrefu na zitafanya kila nyimbbo kwenye album zionekani ni kali.


Mwaka huu 2021 unaweza kuwa mzuri sana kwa Darasa kimziki kutokana na aina ya nyimbo zilizo kwenye album yake kwani nyingi zitakaa sana masikioni mwa watu na zitakuwa pendwa sana kwenye sehemu za starehe na kila eneo la burudani na bahati aliyonayo Darasa hafungamani na upande wowote hasa kwenye media na wadau wa Sanaa kwa hiyo ni wazi atafanya vyema.




Nilipata wasaha wa kusikiliza kila wimbo kwenye Album ya Darasa na kuuchanganua…..


Proud of You ft Alikiba- Kwenye huu wimbo Alikiba kautendea haki sana na ninachelea kusema huu ni hit kabisa na alivyo ingia darasa kipande chake ndio kimefanya huu wimbo upendeze sana na huu nina hakika ndio wimbo pendwa kabisa mtaani na sehemu nyingi… huu ni wimbo namba moja kwenye album lakini pai mimi nauita ni hit song namba moja kwa mwaka huu……


Umeniroga ft Kassim Mganga-Ukisikiliza huu wimbo utakubaliana nami kuwa huu utakuwa wimbo namba mbili kuwa hit song kutoka kwenye album ya darasa kwani kwenye hii album huu wimbo ndio umekuwa na chorus bora kabisa kutoka kwa Kassim Mganga ,humu Kassim Mganga kaimba kipande kidogo tena chorus lakini ukisikiliza utotamani amalize chorus au utatamani angepewa nay eye ubeti mmoja….humu kassim Mganga kaua sana chorus na darasa kama kawaida yake anavyo ingia kwenye beat aisee ni hatari sana


Namnukuu Kassim Mganga anase “ Ukicheka ukinuna,ukisema ukiguna,mzuri wa sura kakujalia mamaaaa Naona, ona kama umeniroga, wanasema umeniroga naamini hujaniroga eeeh”


Ni wimbo namba 3 kwenye album lakini utakuwa namba mbili kuwa hit ,ukisikiliza unaweza ukafikiri ni beat nyimbo za Christmas……


Loyality ft Mario and Nandy. Huu nao utakuwa namba tatu kuwa hit trust me maana humu wamekutana mafundi tupu na auchoshi kuwasikiliza ….. humu Mario na Nandy wamemfunda vizuri darasa hawa vijana…..kama kawaida yao Mario na Nandy kwakweli niwape hongera sana wameitendea kazi sana hii track na bila shaaka itakuwa hit….lakini Marioo jamani ni habari nyingine.Huu ni wimbo namba tano kwenye album ya Darasa lakini utakuwa wimbo wa tatu kuwa hit kutoka kwenye album yake….



Hands up ft Maua sama utakuwa wimbo wa nne kuwa hit kutoka kwenye album ya darasa japo ni wimbo namba 10 kwenye album lakini ni wimbo mzuri sana kifupi ni club banger ….humu maua ameingiza sauti na amefanya wimbo upendeze….


Shemeji ft Baraka Da Prince hii nayo ni hit namba tano japo ni wimbo namba 17 ,Humu Baraka karudi kwenye ubora wake kabisa akimsihi shemeji yake kuwa asimchezee dada yake, lakini Darasa ana msihi kuwa asiwe na wasi kwani yeye ni mnyamwezi kabisa na yuko serious … ni wimbo mzuri sana.


Segedance ft Rich mavoko huu ni wimbo wa sita hit japo ni wimbo namba 17 kwenye album ni wimbo ambao Rich mavoko ameutendea haki sana kwenye chorus auchoshi kusikilizwa hakika humu mavoko katulia sana.


Nimetumwa pesa ft Bill nas and Ben pol…..Hii ni hit song namba saba ninajua ukitoka utatamba sana na utakuwa wimbo pendwa sana kwa vijana na watu wengi kwani title tuu umeubeba wimbo….huu wimbo unahamasisha kutafuta pesa ni wimbo mzuri sana………


Kimsingi Album ya Darasa ni album bora namba mbili kwa sasa ukiacha album ya Harmonize Darasa anatarajiwa kufanya vyema sana mwaka huu 2021 na nyimbo zake zitatamba sana…..


Bado hadi sasa Album ya Harmonize inaongoza kuwa na hit songs nyingi kuliko album nyingine za wasanii wa bongo fleva na ninaipa nafasi ya pili kuwa na hit song nyingi pia japo bado hijaingia mtaani kwani ni mapema sana lakini ni wazi itafanya vyema.


Kituo kinacho fata ni Album ya BARNABA –ASANTE NA ALBUM YA JUX-FASHION KILLER nazo tutazichambua


Wasalaam……