Serikali ya Ujerumani imetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya maabara zinazoshindwa kuwasilisha chanjo dhidi ya virusi vya corona kulingana na ratiba ya Umoja wa Ulaya. 

Ujerumani inatishia kuchukua hatua hii huku kukiwa na wasiwasi juu ya kucheleweshwa kwa usambazaji wa chanjo za AstraZeneca. Waziri wa uchumi wa Ujerumani Peter Altmier amsema hayo alipozungumza na gazeti la kila siku la Ujerumani la Die Welt.

Kumekuwepo na kuongezeka kwa hali ya wasiwasi katika wiki za hivi karibuni kati ya viongozi wa Ulaya na kampuni kubwa ya madawa ya AstraZeneca, ambayo imesema haitaweza kuwasilisha kiwango cha chanjo ilichokiahidi kwa Umoja huo hatua iliyoazua mzozo huku baadhi ya mataifa kama Italia yakiahidi kuichukulia hatua za kisheria.