Tume ya uchaguzi nchini Uganda imepiga marufuku wapiga kura kwenda na simu au kamera kwenye kituo cha kupiga kura wiki ijayo tarehe 14 au kubaki kituoni kusubiri matokeo, agizo hilo limetolewa jana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Simon Byabakama mjini Kampala.

Huku mashirika yasiyo ya serikali yakitaka tume kufafanua kuhusu teknolojia itakayotumiwa katika uchaguzi mkuu zikiwa zimesalia siku saba kufanyika zoezi hilo.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Uganda Jaji Simon Mugenyi Byabakama ametangaza kanuni zitakazotumiwa katika uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku wandishi habari kuingia ndani kwenye vituo vya kupiga kura ,kuvaa sare za chama chochote cha siasa au za mgombea yoyote, simu za mukononi pamoja na kamera kama anavyoelezea:

Agizo la Jaji Byabakama kuzuia wapiga kura kubaki kwenye vituo vyao vya kupiga kura zinakinzana na zile za baadhi ya wagombea wa kiti cha rais ambao wamesikika katika kampeni zao za uchaguzi wakiwataka wafuasi wao baada ya kupiga kura wabaki kituoni kulinda kura zao.

Mwenyekiti wa tume ameongeza kuwa wapiga kura wakibaki kwenye vituo vya kupiga kura watasababisha msongamano mkubwa wa watu na kuvunja kanuni za watalaam wa afya za kudhibiti virusi vya corona.

Wakati huo mashirika yasiyo kuwa ya serikali wamelaumu tume ya uchaguzi kushindwa kutowa elimu kwa wapiga kura, pia wameitaka tume hiyo kuelezea wananchi ni teknolojia gani watakayotumia ili kuhakikisha uchaguzi huru na haki ambao matokeo ya uchaguzi