Mgombea wa wa chama cha Democratic Raphael Warnock ameibuka mshindi katika uchaguzi wa maseneta dhidi ya mgombea wa chama cha Republican Kelly Loeffler katika jimbo la Georgia, kulingana na vituo vya habari vya CNN, CBS na NBC leo Jumatano, Januari 6.

Raphael Warnock, mchungaji wa kanisa huko Atlanta ambapo Martin Luther King alifanya kazi, ataandika historia kwa kuwa seneta wa kwanza mweusi aliyechaguliwa katika jimbo hili la kusini.

Chama cha Democratic kinatarajia kushinda uchaguzi mwingine mdogo wa maseneta katika jimbo la Georgia kuchukua udhibiti wa Bunge la Seneti

Hili ni suala kubwa kwa utawala wa Joe Biden, ambaye atakabidhiwa madaraka Januari 20.

Donald Trump alikuja kuwaunga mkono maseneta wawili kutoka chama cha Republican wanaomaliza muda wao ambao wanawania nafasi zao katika Bunge la Seneti Jumanne hii, Januari 5.

Donald Trump anaendelea na msimamo wake wa kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi mpinzani wake kutoka chama cha Democratic, Joe Biden.


Hata hivyo, matokeo ya kura yalihesabiwa mara kadhaa huko Georgia na ni wazi: Joe Biden ndiye ambaye alishinda uchaguzi wa urais na ndiye ambaye alishinda katika jimbo hili kwa kura 12,000 dhidi ya Donald Trump.