Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kilimanjaro inamshikilia Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Peter Albert Moshi kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Ngono.

Askari huyo alikuwa akichunguza ajali ya pikipiki ambayo ilimgonga mtoto na kusababisha kuvunjika mkono. Aliomba Rushwa Ngono kwa mama wa mtoto ili aweze kukamilisha Taarifa za Uchunguzi.

Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Kilimanjaro, Frida Wikesi amesema, askari huyo amekamatwa Januari 6 akiwa nyumba ya kulala wageni maeneo ya Soweto Mjini Moshi.

Uchunguzi wa TAKUKURU umebaini kuwa, Peter alimsumbua mama wa mtoto kwa muda mrefu na hivyo kusababisha shauri kuchelewa hali iliyopelekea mama huyo kupeleka malalamiko na wakaweka mtego wa kumkamata.