Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kwa miezi sita kituo cha teloevisheni cha Wasafi kwa kosa la kukiuka kanuni za utangazaji katika matangazo yake ya moja kwa moja ya tamasha la ‘Tumewasha na Tigo’.
Uamuzi huo umefikiwa leo Jumanne Januari 5 baada mamlaka hiyo kukutana na uongozi wa Wasafi TV na kusikiliza utetezi wao.
Kaimu Mkurugenzi wa TCRA, Johanes Kalungule amesema ukiukwaji huo ulifanyika Januari 1, 2021 ambapo televisheni hiyo ilirusha maudhui yaliyomuonyesha msanii Gigy Money akicheza katika mitindo iliyoonyesha utupu wake.
Kalungule amesema kosa hilo ni kinyume na kanuni za utangazaji, hivyo kuanzia muda uliotolewa uamuzi huo Wasafi TV imetakiwa kusitisha matangazo yake na kuomba radhi mfululizo.