Warembo wawili kutoka Marekani, wamejikuta wakimuingiza Tajiri namba moja barani Afrika, #AlikoDangote kwenye headlines za vyombo mbalimbali vya habari Afrika baada ya kuweka mambo hadharani kwenye mitandao ya kijamii, kisa kikiwa mmoja wao kuibuka na kudai kuwa mahusiano yake na #Dangote yamemfundisha mambo mengi.


‘Vurugu’ yote ilianza baada ya mwanadada mmoja aliyetambulika kwa jina la Bea Lewis kupost katika ukurasa wake wa Instagram, picha iliyomuonesha akiwa na #AlikoDangote, ikisindikizwa na video clips kadhaa zikimuonesha akiwa ‘batani’ na tajiri huyo mwenye asili ya Nigeria, picha iliyosindikizwa na maneno yaliyosomeka.....


“Nimekuwa katika mahusiano na mwanaume tajiri mweusi duniani, ameuvunja moyo wangu katika vipande 1,000, nimejifunza mengi kutoka kwake, nimejifunza kufanya vitu katika mpangilio na kujitegemea, na hatimaye nimeepuka ratiba za kuwepo jikoni kila wakati”


Ndipo mrembo mwingine aliyefahamika kwa jina lake la Instagram kama @allarounda1 akaja juu akidai kuwa #BeaLewis hajawahi kuwa na mahusiano na #Dangote, huku akionesha uthibitisho wa jumbe zinazosadikiwa kuwa zimetoka kwa #Dangote mwenyewe akikanusha kuwa na mahusiano na mrembo huyo, jumbe hizo zilisomeka, “Sio tu anatafuta ‘kiki’ ila pia ni mwizi mwenye njaa”, “Sijawahi kuwa na mahusiano naye”, 


Kupitia insta story, @allarounda1 aliandika jumbe nyingi na mojawapo ilisomeka “@iambealewis umekuwa ukitamani kujitangaza muda mrefu sana, nipo hapa kusafisha jina lake (la Dangote), kitu ulichofanya kinachefua na si cha kufumbia macho”


Hii si mara ya kwanza kwa #Dangote kuwahi kuhusishwa  na skendo za mahusiano, mwaka 2019 aliwahi kushutumiwa kumpigia ‘pasi ya goli’ Monica Musonda kuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika program ya kuthibiti utapiamlo, ikiwa imepita miaka michache tangu wawili hao kudaiwa kuwa katika mahusiano baada ya picha yao wakibusiana kuvuja.