Dudu baya kizimbani kwa kutoa lugha chafu

Mwanamuziki wa Bongofreva, Godfrey Tumaini maarufu 'Dudu baya' amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shtaka la lugha chafu mtandaoni.

Dudu baya (41) Mkazi wa Mbezi amepandishwa kizimbani jana na kusomewa hati ya Mashitaka na Wakili wa Serikali, Hilda Katto mbele ya Hakimu Mkazi, Ester Mwakalinga.

Wakili Katto amedai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 11, mwaka 2020 akiwa nchini Tanzania 

Aliendelea kudai, mshtakiwa Dudu baya aliandika lugha ya matusi kwa Joseph Kusaga katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kuisambaza, ambapo aliandika kuwa "mbabewavita......,msemakweli.....,mfungwahuru.....,wafanyakazi wake pale wasafi Ni mustaph(hr)na Nelly(program maneger)na leseni ya wasafi media imesajiliwa na Zanzibar anapotokea mke wake ....waulize TCRA kama nasema uongo...., Joseph anatumikishwa kuzalisha mashoga Tanzania.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo, kwa upande wa Jamhuri wakili amedai upelelezi umekamilika na kuiomba mahakama kupanga tarehe kwa ajili ya kusikilizwa.

Dudu baya yuko nje kwa dhamana hadi Januari 28, kesi hiyo itakapotajwa tena.