Hatimaye mmliki wa chombo cha habari cha Wasafi TV, msanii Diamond Platnumz ameandika ujumbe wake wa kwanza tangu kituo chake cha runinga kifungiwe kurusha matangazo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA.

Ikumbukwe, Wasafi TV imefungiwa kutoa huduma kwa muda wa miezi 6 kuanzia Januari 6 mwaka huu hadi Juni 2021 kwa kosa la kukiuka kanuni za utangazaji katika matangazo yake ya moja kwa moja ya tamasha la Tumewasha.

“Mwenyezi Mungu amekupa nafasi ili nawe kuwapa wenzio fursa waweze kujikwamua kimaisha, sio kila utayempa nafasi atakuletea Matokea Chanya. Usihuzunike, kubaliana na hilo na uendelee kutoa Misaada, kuwapenda na kuwaheshimu wote,” ameandika Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kwa kuanisha zaidi, chanzo kilikuwa ni kivazi alichovaa msanii #GigyMoney wakati akitumbuiza katika Tamasha hilo.