Simba Sport Club leo January 22, 2021 , imetangaza michuano ya Kimataifa ‘Simba Super CUP’ ikihusisha timu tatu Simba, TP Mazembe ya Congo na Al Hilal ya Sudan,


Pia, timu hiyo imesema, kesho Jumamosi, itamtangaza kocha mpya atakayechukua mikoba ya Sven Vanderbroeck aliyeondoka. Kocha mpya atasaidiwa na kocha msaidizi, Suleiman Matola.

Akitangaza michuano hiyo leo Ijumaa tarehe 22 Januari 2021, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba (CEO), Barbara Gonzalez amesema, michuano hiyo, itaanza Jumatano ijayo tarehe 27- 31 Januari 2021.

Amesema, mechi ya kwanza itakuwa Simba dhidi ya Al Hilal saa 11 jioni.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema, michuano hiyo “ni maalum kwa mabingwa wa nchi, kama timu yako siyo bingwa, huhusiki na michuano hii.”