Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, akizungumza leo na wanahabari jijini Dar es Salaam, amefunguka mambo mengi kuhusu klabu hiyo pamoja na sakata zima la kiungo mzawa Jonas Mkude.

Haya hapa kati ya yale aliyozungumza leo kuhusu Simba pamoja na sakata la Mkude kusimamishwa ndani ya klabu hiyo.


"Mechi ya Simba na Platinum itachezwa saa 11 jioni siku ya tarehe 6 mwezi januari".


"Kama sisi tukifuzu makundi mwaka huu, msimu wa 2022/23 Tanzania tutawakilishwa na timu 4 kwa sababu nafasi ya Libya haitokuwepo. Sasa unaombeaje sisi tutolewe halafu unajiita mzalendo? Kaa nyumbani tu haisaidii"


"Simba SC haijawahi kufanya vizuri kimataifa bila sapoti kubwa ya mashabiki. Simba ni klabu ya watu sio klabu ya wananchi wala wazalendo. Bila watu Simba pale kwa mkapa sio kitu. Lakini mashabiki wakitoa sapoti kubwa Platinum hawatoki. Tukaimbe wida wida wida" amesema Haji Manara.


Kuhusu Mkude, ofisa habari huyo amesema, "Mkude ni mchezaji wa Simba SC. Jambo lake lipo kamati ya maadili. Mkude hajafukuzwa Simba SC. Bila shaka yoyote baada ya kamati atarejea klabuni. Huyu ndiye mchezaji mwandamizi ndani ya Simba kwa miaka 10"


"Hakuna mwanadamu ambaye hakumbani na changamoto. Anayokutana nayo ni Mkude ni ya kawaida."


Aidha, Hajis Manara aliongeza, "Ilimradi wewe ni mtu, Simba ndio klabu yako. Hata uwe mfugaji, uwe mzalendo au mwananchi timu yako ni Simba SC"


"Kuna jarida limejiridhisha kuwa penye watanzania 10 watanzania 7 ni mashabiki wa Simba SC" ameeleza Manara.