Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limekamilisha ujenzi wa miundombinu ya umeme itakayotumika kuendesha treni ya mwendokasi (SGR) kutoka jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro huku awamu ya pili kutoka mkoani Morogoro kuelekea Matukupola mkoani Dodoma ikitarajiwa kuanza hivi karibuni.

Akizungumza mjini Morogoro mara baada ya kutembelea kituo cha kupozea umeme kilichopo Kingolwira nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kwa sasa ujenzi wa miundombinu hiyo yenye urefu wa kilomita 160 imekamilika kwa asilimia 100.

Kwa upande wake Meneja Mwandamizi wa miradi kutoka TANESCO, Mhandisi Emmanuel Manilabona amesema vituo vyote vya kupoza umeme vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro tayari vimeshakalimika.