Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez ametangaza kuwa ameambukizwa virusi vya Corona usiku wa kuamikia leo, kwa muda mrefu Kiongozi huyo ameonesha kutolipa uzito janga la Corona na mara nyingi huonekana hadharani bila ya kuvaa barakoa.
Lopez ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba amegundulika kuwa na maambukizi ya Corona lakini anaonesha dalili za kawaida na tayari ameanza kupatiwa matibabu.
Amesema ana matumaini ya kupata nafuu na ataendelea na shughuli za kila siku za kuongoza Taifa ikiwa ni pamoja na mazungumzo ya simu na Rais Vladimir Putin wa Urusi yaliyopangwa kufanyika baadaye leo.
Mexico imepoteza zaidi ya watu 149,000 kutoka na ugonjwa wa COVID-19 na kuwa Taifa la nne duniani kwa idadi kubwa ya vifo tangu kuzuka kwa janga hilo mwishoni mwa mwaka 2019.