Rais wa Marekani Joe Biden leo anatarajiwa kutangaza marufuku ambayo itawazuia kuingia Marekani Raia ambao sio Wamarekani kutoka Uingereza, Ireland, Brazil na Mataifa mengi ya Ulaya.
Biden pia ataongeza muda wa zuio kwa Watu ambao wamesafiri kwenda Nchini Afrika Kusini siku za karibuni nao hawatorushiwa kuingia Marekani.
Kirusi Kipya cha Corona kilichobainika Afrika ya Kusini kimeonesha kuwa ni hatari zaidi kuliko virusi vilivyo katika Nchi nyingine Duniani na kimeonekana kuathiri zaidi wagonjwa wengi nchini Afrika ya Kusini na husambaa kwa haraka zaidi kuliko hata kile kirusi kipya kinachopatikana Uingereza.
Kutokana na Kuwepo kwa kirusi hicho Afrika ya Kusini, Nchi nyingi zimezuia safari za ndege kuingia na kutoka Nchini humo.