Rais wa #Tanzania, Dkt. John Magufuli amempongeza Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa kuchaguliwa na kutangazwa na Tume ya Uchaguzi ya #Uganda kuwa mshindi wa Nafasi ya Urais


Rais Magufuli amesema, Tanzania itaendeleza urafiki na udugu uliopo kwa maslahi mapana ya Wananchi. Pia, amewapongeza waganda kwa kumaliza Uchaguzi Mkuu kwa Amani


Januari 16, Tume ya Uchaguzi ya Uganda ilisema Yoweri Museveni amepata Kura 5,851,037 sawa na 58.64% akifuatiwa na Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) akipata Kura 3,475,298 sawa na 34.83%