MAKOCHA 10 wameishia njiani ndani ya Ligi Kuu Bara mpaka sasa kutokana na sababu mbalimbali kwa msimu wa 2020/21.

Hawa hapa kazi yao haikufika mwisho namna hii:-

Zlatko Krmpotic wa Yanga alifutwa Oktoba 3 kwa sasa nafasi yake ipo chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

Maka Mwalwisi alifutwa kazi ndani ya Ihefu, Oktoba 6 nafasi yake ipo mikononi mwa Zuber Katwila.

Khalid Adam wa Mwadui FC alibwanga manyanga ndani ya kikosi hicho na sasa nafasi yake ipo mikononi mwa Amri Said.



Zuberi Katwila alibwaga manyanga ndani ya Mtibwa Sugar, Oktoba 18 nafasi yake ipo mikononi mwa Hitimana Thiery.

Amri Said alifutwa kazi ndani ya Mbeya City Oktoba 21.

Hitimana Thiery wa Namungo alifutwa kazi Novemba 21, nafasi yake ipo mikononi mwa Hemed Morroco.

Arstica Cioaba wa Azam FC alifutwa kazi Novemba 26 nafasi yake ipo mikononi mwa George Lwandamina.

Fulgence Novatus aliyekuwa Kocha Mkuu wa Gwambina na msaidizi wake Athuman Bilal walifutwa kazi ndani ya Gwambina FC Januari 4.

Sven Vandenbroeck, ndani ya kikosi cha Simba aliachia ngazi Januari 7.