MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Yanga, Saido Ntibazonkiza amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2020/21
Saido ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda kiungo Clatous Chama wa Simba na kiungo mshambuliaji wa Dodoma Jiji FC, Seif Karihe alioingia nao fainali.

Saido alionesha uwezo mkubwa katika michezo mitatu aliyocheza na kuwa msaada mkubwa kwa Yanga, ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mawili na kutoa pasi za mwisho tatu zilizozaa mabao. Saido amesajiliwa Yanga katika dirisha dogo la usajili lililofunguliwa katikati ya mwezi uliopita.