Mlinzi wa kushoto wa klabu ya Yanga, Yassin Mustapha Salum amesema kitendo cha kuitwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania kwa wachezaji wanaocheza ndani kwajili ya michuano ya CHAN, ni kutimiza ndoto yake ya muda mrefu.

 

''Kikubwa mimi nimefurahi sana na ninashukuru maana ndoto yangu imetimia kwasababu mchezaji hauwezi kuwa kamili bila kucheza timu ya taifa, hivyo kwangu kupata hii nafasi ya kuitwa miongoni mwa wachezaji 30 ni heshima kubwa'', amesema.


Aidha Yassin ameongeza kuwa, ''mimi nawaomba watanzania waachane na mambo yote ya nje ya uwanja na watuunge mkono na kutupa nguvu maana hii ni timu ya taifa''.


Yassin Mustapha ameitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Taifa Stars kitakachoshiriki michuano ya CHAN 2021 nchini Cameroon kuanzia Januari 16, 2021.