BADO kelele za ndoa ya staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mchumba wake wa siku nyingi, Francis Siza almaarufu Majizo kutofungwa zinasikika huku nyuma yake kukiwa na siri nyingine mpya, Risasi Mchanganyiko limedokezwa.

Matangazo ya kufungwa kwa ndoa ya Lulu na Majizo yalidaiwa kusikika katika Kanisa Katoliki la Mbezi-Beach jijini Dar, mwezi Oktoba, mwaka jana.

 

ILIPANGWA KUFUNGWA NOVEMBA 2

Kwa mujibu wa matangazo hayo, ndoa ya Lulu na Majizo ilipangwa kufungwa Novemba 2, mwaka jana, lakini ghafla kukaibuka sintofahamu.Baada ya hapo kumekuwa na fukuto la jambo hilo kutotimia kwa matarajio hayo ya mashabiki wengi wa Lulu.



LULU: TUIPE MITANO TENA

Hata hivyo, kila mara Lulu amekuwa akitoa majibu tata juu ya kutofungwa kwa mara nyingine.“Tuipe mitano tena,” Lulu alimjibu mmoja wa wafuasi wake kwenye Mtandao wa Instagram aliyemhoji ndoa yake hiyo itafungwa lini.

 

RISASI MZIGONI

 

Katikati ya sintofahamu hiyo ndipo Gazeti la Risasi Mchanganyiko, mwishoni mwa wiki iliyopita likaingia mzigoni kutafuta mbivu na mbichi.Gazeti hili lilifika kwenye kanisa hilo na kuomba kuonana na Paroko, lakini hakuwepo.

 

INAWEZEKANA KUFUNGWA KWINGINE

 

Hata hivyo lilizungumza na mmoja wa Padri aliyeomba hifadhi ya jina kwa kuwa siyo msemaji wa kanisa hilo ambaye alisema inawezekana ndoa hiyo ilikwenda kufungwa sehemu nyingine.

 

Alisema kuwa, mafunzo yanaweza kutolewa kanisani hapo, lakini ndoa ikawa imekwenda kufungwa kwenye Kanisa Katoliki lingine na ni utaratibu uliozoeleka hivyo hawezi kusema kama ilifungwa mahali hapo au pengine.Hata hivyo, wakati gazeti hili linataka kuondoka kanisani lilikutana na mtu mwingine ambaye alieleza anachokijua juu ya kutofungwa kwa ndoa hiyo.



SAFARI YA NIGERIA YATAJWA

Alisema kuwa, ni kweli matangazo yalikuwa yakitolewa kanisani hapo, lakini kabla ya kuhitimisha semina ya ndoa, Lulu aliomba hudhuru wa kusafiri na baada ya hapo hakurejea kuendelea na semina kisha kufunga ndoa hiyo.“Kama nitakumbuka vizuri, Lulu alipoomba udhuru alisafiri kwenda Nigeria, lakini aliporejea nchini sikujua nini kiliendelea…” Kinasema chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina na kusisitiza kuwa ndoa hiyo haijafungwa mpaka kesho.

 

VUGUVUVUU LA NDOA YA LULU

Kabla ya matangazo ya ndoa hiyo kanisani, vuguvugu la ndoa hiyo liliibuliwa na Majizo ambaye kupitia ukurasa wake wa Instagram, alitupia picha akiwa na Lulu na kuandika; “Comments zihusu ukumbi gani utatosha!”Posti hiyo iliamsha utamu uliokuwa umekata wa ndoa yao ambayo ilikuwa imesubiriwa zaidi ya miaka mitatu na kuonekana kama usanii.

 

Hata hivyo, baada ya kutangazwa kanisani, matumaini ya wengi yalifufuliwa na watu kuishia kusema; “Hatimaye hayawi…hayawi yanakwenda kuwa…”Kwa mujibu wa taratibu za Kanisa Katoliki, kabla ndoa haijafungwa, ni sharti itangazwe kwa majuma matatu mfululizo na ndicho kilichofanyika, lakini jambo la wawili hao halikutimia.

TULIKOTOKA

Lulu na Majizo wamekuwa wakijiiba kimapenzi kwa muda mrefu, ambapo Septemba 2018, uchumba wao uliingia kwenye hatua ya kuvishana pete ya uchumba kisha wakatulia zao.Tangu hapo, hawaoani…hawaoanizikawa nyingi hadi kufikia hatua ya uzushi kuenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba, Majizo ameamua kubadili gia angani na kuachana na Lulu.

 

Mara nyingi wawili hao, wamekuwa kama wanacheza na akili za watu, kwa kuacha kila lisemwalo juu yao mitandaoni na kwenye vyombo vya habari lipite bila majibu yao kuhusu ndoa yao

 

.Kabla ya Lulu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Majizo, alikuwa akitoka na aliyekuwa kinara wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba, ambaye baadaye aliingia matatani kwa kuhusika na kifo chake.Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 kwa kile kinachotajwa kuwa, ni baada ya kutokea ugomvi kati yake na Lulu, ambaye alikwenda nyumbani kwa Kanumba usiku wa tukio.

 

Kufuatia kifo cha Kanumba, Lulu aliingia kwenye msukosuko wa kisheria, hadi Novemba 2017 alipokutwa na hatia ya kuua bila kukusudia na mahakama kumfunga jela miaka miwili.

Hata hivyo, Mei 12, 2018, staa huyo alitoka jela na kutakiwa kumalizia kifungo chake kwa kufanya kazi za kijamii kwa amri ya Mahakama Kuu.Kufuatia mauaji hayo ya Kanumba, Lulu alijikuta kwenye mgogoro na mama Kanumba, Flora Mtegoa.

 

Mara kadhaa mama Kanumba alinukuliwa akimlaani Lulu, kwa kile alichokuwa akikitaja kuwa ni kuhusika kwake na kifo cha mwanaye na baadaye kujitenga naye